Zuma hana kinga ya kutoshtakiwa – Ramaphosa

Muktasari:

Wabunge waliliambia shirika la News24 kwamba Ramaphosa alitaka kuondokana na uvumi katika vyombo vya habari kwamba mkutano wake na Zuma Jumanne ulihusu kumlinda ili asiweze kukabiliwa na mashtaka ya rushwa.


Cape Town - Rais wa ANC, Cyril Ramaphosa amewaambia wabunge wa chama chake hicho kwamba kinga ya kutoshtakiwa Rais Jacob Zuma si sehemu ya mazungumzo juu ya serikali "ya mpito".

Pia, aliwahakikishia wabunge kuwa mazungumzo hayo yatahitimishwa katika muda wa "siku moja au mbili" zijazo.

Ramaphosa alihutubia kikao cha wabunge wa chama hicho tawala Alhamisi, akiwa na katibu mkuu wa chama Ace Magashule na mnadhimu mkuu Jackson Mthembu.

Mkutano ulionekana kuwa wa dharura, hasa kutokana na ANC kufanya vikao vya wabunge baada ya rais kulihutubia taifa hotuba ambayo huonekana kuwa ni ufunguzi rasmi wa Bunge.

"Kinga ya kutoshtakiwa wala haiko kwenye majadiliano mezani. Haiko katika mamlaka yangu," vyanzo vilimnukuu Ramaphosa akisema.

 

Wabunge waliliambia shirika la News24 kwamba Ramaphosa alitaka kuondokana na uvumi katika vyombo vya habari kwamba mkutano wake na Zuma Jumanne ulihusu kumlinda ili asiweze kukabiliwa na mashtaka ya rushwa.

Mkurugenzi wa Taifa wa Mashtaka ya Umma, Shaun Abrahams bado anahitaji kuamua ikiwa atarejesha mashtaka ya udanganyifu na rushwa dhidi ya Zuma.

Zuma pia ni mtuhumiwa katika uchunguzi unaofanywa wa serikali kuwekwa mfukoni inayoongozwa na Naibu Jaji Mkuu Raymond Zondo. Ana uwezo wa kupendekeza kwamba wale waliotajwa wanapaswa kukabiliwa na mashtaka ya jinai.

"Yaye (Ramaphosa) alisisitiza kwamba hakuweza kufanya kitu chochote kinyume cha sheria, au kuzungumza na Zuma juu ya kitu chochote ambacho hakiko ndani ya mamlaka ya utendaji." Alisema hakuweza kuingia katika nafasi hiyo, "alisema mbunge mmoja.