Rammy azungumzia mahusiano yake na Masogange

Muktasari:

  • Rammy na Masogange walipanga kuzindua filamu baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Msanii wa filamu Rammy Galis, amezungumzia mahusiano yake  kimapenzi na ‘video queen’ Agnes Gerald, maarufu Masogange.

Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 22, 2018 katika viwanja vya Leaders Club wakati wa kuaga mwili wa Masogange, amesema mahusiano yao yalianza mwaka 2016 na yalivunjika mwaka 2017.

“Ameniachia vidonge mwilini mwangu,  licha ya kuachana tulibaki kuwa marafiki wa karibu,” amesema.

Galis amesema urafiki wao uliendelea hadi wakaamua kucheza pamoja filamu iitwayo ‘Hukumu’.

Kwa mujibu wa Rammy, filamu hiyo imeshakamilika na walipanga kuizindua baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza Mei, 2018.

Masogange alifariki dunia Ijumaa Aprili 20, 2018 katika Hospitali ya Mama Ngoma, iliyopo Mwenge.