Rangi za pilipili hoho kila moja ina faida yake mwilini

Wengi tunafahamu kuwa pilipili hoho ni kiungo cha mboga katika mapishi mbalimbali, lakini hatufahamu kama ni miongoni mwa mboga yenye vitamin nyingi, achilia mbali uwezo wa kuboresha mifumo ya mwili. Pilipili rangi ya njano ndio mboga pekee yenye zeaxanthin kwa wingi kuliko mboga yeyote ikifuatiwa na Mahindi inayoshika nafasi ya pili.

Hata hivyo, Hoho au Sweet pepper kwa jina la kitaalamu inauwezo wa kuongeza kinga ya mwili pamoja na kupambana na magonjwa ya saratani, moyo huku ikisaidia kuboresha uwezo wa macho kuona vizuri.

Mbali na kuwa kiungo kutumika katika mboga ua kachumbari na wakati mwingine hutumika kama saladi, Hoho kutumika kwa kutengeneza juice ambayo husaidia kutoa taka mwili. Hoho hupatikana katika muonekano wa rangi tofauti ambazo ni rangi nyekundu, kijani, urujuani na njano na zinatajwa kuwa mboga yenye vitamin zaidi ya 30. Miongoni mwa faida zilizopo katika hoho ni kwamba hutibu kuwasho wa koo na vidonda vilivyopo kooni, hutibu watu wanaotoka damu puani na huimarisha kinga ya mwili kutokana na wingi wa vitamibi C iliyopo ndani ya kiubgo hicho ambacho hupigana dhidi ya magonjwa na kujenga kinga imara. Hoho husaidia watu wenye shida katika mfumo wa upumuaji kutokana na kuwa na vitamin C nyingi, hukinga dhidi ya magonjwa ya kansa ya kibofu cha mkojo na ugonjwa wa baridi yabisi. Husaidia kupunguza uzito , kuboresha mzunguko wa damu na kupunguza kolesto mwilini kwa sababu ina kiwango kidogo cha kalori na pia huzuia shinikizo la damu na kutibu anemia. Hutibu kuhara, ugonjwa wa homa ya manjano, hurekebisha presha ya kupanda na husaidia katika mmengenyo wa chakula kufanyika vizuri. Kwa wale wanaosumbuliwa na gesi tumboni wanashauriwa kutengeneza juisi ya pilipili hoho wakichanganya na juisi ya spinachi. Pilipili hoho rangi ya njano ikitumika vizuri katika mapishi ni mboga yenye faida nyingi kiafya achilia mbali ladha ya kipekee, ina uwezo mkubwa ya kuboresha mifumo mbalimbali mwilini na ndio mboga pekee yenye zeaxanthin kwa wingi kuliko mboga yeyote ikifuatiwa na Mahindi inayoshika nafasi ya pili. Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya afya wanasema hoho rangi ya njano ni chanzo kizuri cha virutubisho aina ya lutein na zeaxanthin ambazo huzuia matatizo ya mtoto wa jicho na udhaifu wa misuli. Pilipili hoho rangi nyekundu (red pepper) inabaki kuwa mojawapo ya vyakula vichache vyenye kirutubisho cha lycopene ambacho hupunguza hatari ya saratani mbalimbali.