Ranieri atimuliwa Leicester

Muktasari:

Tukio Hilo lililoshtua wengi limetokea miezi 9 baada ya kuipa ubingwa timu hiyo ambayo hata uchumi wake umeelezwa kuporomoka tofauti na awali.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England,wamemfukuza kazi kocha aliyewapa ubingwa, Claudio Ranieri.

Tukio Hilo lililoshtua wengi limetokea miezi 9 baada ya kuipa ubingwa timu hiyo ambayo hata uchumi wake umeelezwa kuporomoka tofauti na awali.

Ranieri, 65, ameshindwa kutamba na timu hiyo msimu huu kwenye Ligi ya Ndani na michuano ya Kimataifa huku akiondokewa na mastaa kadhaa.