Risasi zarindima mahakamani Kisutu

Muktasari:

Washtakiwa hao ambao ni viongozi na wafuasi wa Uamsho walikuwa wakisafirishwa katika basi la Magereza lililokuwa likisindikizwa magari aina ya  Land Rover Defender zilizokuwa zimejaa askari wenye silaha na baadhi yao wamejifunga vitambaa vyeusi usoni.

Dar es Salaam.  Polisi waliokuwa wanawasindikiza washtakiwa wa kesi ya ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana walilazimika kufyatua risasi hewani wakati wa kuwaingiza na kuwatoa mahakamani hapo.

Washtakiwa hao ambao ni viongozi na wafuasi wa Uamsho walikuwa wakisafirishwa katika basi la Magereza lililokuwa likisindikizwa magari aina ya  Land RoverDefender zilizokuwa zimejaa askari wenye silaha na baadhi yao wamejifunga vitambaa vyeusi usoni.

 Risasi hizo ziliwatawanya ndugu wa washtakiwa hao wanaofika na kukaa nje kila kesi hiyo inapotajwa walipotaka kusogelea msafara huo.

Washtakiwa hao ni Sheikh Farid  Hadi Ahmed,  mkazi wa Mbuyuni;  Noorid Swalehe wa Fundi ujenzi , mkazi wa Koani  na  Jamal  Nooridin  Swalehe.

Wengine ni Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally na Juma Juma.

Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu.

Inadaiwa kuwa  kati ya Januari 2013 na Juni 2014  walipanga njama  za kusaidia na kuwezesha kufanyika kwa vitendo vya kigaidi.