Friday, September 14, 2018

Rita yaeleza sababu wanawake kuwazidi akili waume usajili wa watoto

aimu meneja wa usajili vizazi na vifo (Rita),

aimu meneja wa usajili vizazi na vifo (Rita),  Patricia Mpuya 

By Phinias Bashaya, Mwananchi pbashaya@mwananchi.co.tz

Bukoba. Iko hivi. Kama una mgogoro na mwenza wako usikubali akajifungue kabla hamjapatana kwa sababu mtoto atakayezaliwa anaweza kusajiliwa kwa jina la baba mwingine na maisha yakaendelea.

Ufafanuzi huo umetolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) katika semina iliyoandaliwa kwa viongozi wa Mkoa wa Kagera leo Ijumaa Septemba 14, 2018 mjini Bukoba.

Rita imetoa ufafanuzi huo baada ya ofisa ustawi wa jamii wa wilaya hiyo, Vivian Roland kuuliza swali akitaka kujua hatima ya watoto watakaosajiliwa na kupewa vyeti baadaye kuthibitika kuwa baba halisi wa mtoto jina lake halitajwi kwenye usajili.

Kaimu meneja wa usajili vizazi na vifo (Rita),  Patricia Mpuya amesema utata huo utamalizwa na vipimo vya vinasaba (DNA), kwa sababu wanazozijua wanawake wakati mwingine huandikisha majina ya baba asiye sahihi kwenye vyeti vya watoto baada ya kujifungua.

Ametaja mwanamke kutoelewa na mumewe wakati akijifungua ni moja ya sababu za kutaja jina la baba mwingine wakati wa usajili wa mtoto.

-->