SMZ yaupongeza Mtandao wa Aga Khan

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi

Muktasari:

Pongezi hizo zilitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwenye Maulid juzi.

Dar es Salaam. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeupongeza Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), kutokana na kazi mbalimbali za kimaendeleo inazozifanya nchini, kupitia taasisi zake mbalimbali.
Pongezi hizo zilitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwenye Maulid juzi.
Balozi Iddi alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Ismailia la Tanzania na kufanyika katika Msikiti wa Jamattin, Upanga jijini Dar es Salaam.
 Katika hotuba yake, Balozi Iddi alisema Mtandao wa Aga Khan umefanya kazi nzuri na nyingi za maendeleo zinazopaswa kuigwa na taasisi na asasi zingine zilizopo nchini.