Saa sita zawavuruga Ded, madiwani

Muktasari:

Hata hivyo, Kyombo alisema madiwani hao wakiongozwa na Van Zeeland na Sadiq wamekuwa wakiendesha vikao vyao vya kisheria vya halmashauri kwa kujilipa posho ya kujikimu, posho za kikao na nauli Sh290,000 kwa madai ya kukaa siku tatu wakati wamekuwa wakikaa kikao cha saa sita kwa siku.

Mvomero. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Florent Kyombo amejikuta katika mgogoro mkubwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jonas Van Zeeland na Mbunge wa jimbo hilo, Suleiman Sadiq baada ya kugoma kulipa posho ya Sh296,000 kwa kikao cha madiwani walichokaa kwa saa sita.

Hata hivyo, Kyombo alisema madiwani hao wakiongozwa na Van Zeeland na Sadiq wamekuwa wakiendesha vikao vyao vya kisheria vya halmashauri kwa kujilipa posho ya kujikimu, posho za kikao na nauli Sh290,000 kwa madai ya kukaa siku tatu wakati wamekuwa wakikaa kikao cha saa sita kwa siku.

Alichanganua kuwa katika Sh240,000 ni posho ya kujikimu, Sh40,000 ni ya kikao na Sh10,000 kwa ajili ya nauli.

“Madiwani wamekuwa wakilazimisha na wakiendesha vikao na kujilipa posho za kujikimu kinyume cha sheria kwa siku tatu wanataka walipwe Sh290,000, wakati ni kwa kukaa kikao cha saa sita huku tukidaiwa na benki kutokana na mikopo yao,” alisema Kyombo.

Mkurugenzi huyo alisema halmashauri hiyo inadaiwa Sh1.27 bilioni, madeni ambayo aliyakuta.