Samia aiomba UNEP kuisaidia Tanzania

Makamu wa Rais, Samia Suluhu ameliomba Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira .

Muktasari:

  • Samia ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na UNEP, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Samia Suluhu ameliomba Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini ambao umesababisha mamia ya ekari za misitu kutoweka kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

Samia ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na UNEP, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema pamoja na Serikali kufanya jitihada kubwa za kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo mpango wa upandaji wa miti kote nchini lakini bado msaada na nguvu zaidi inahitajika kutoka UNEP ili kuongeza kasi ya kukabiliana na tatizo hilo nchini.