Samia amuaga balozi wa Israel

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

Makamu wa Rais amesema anafurahi kuona idadi kubwa ya watalii kutoka Israel wakija nchini ambako wa Israel nchini  amesema watalii hao wanavutiwa na mazingira ya Tanzania.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini anayemaliza muda wake, Yahel Vilan.

Balozi huyo alikutana na Makamu wa Rais na kumuaga rasmi kwani muda wake wa kutumikia nchini ulikuwa umemalizika.

Makamu wa Rais amesema anafurahi kuona idadi kubwa ya watalii kutoka Israel wanaokuja Tanzania.

“Tunawakaribisha sana Tanzania, waje kwa wingi wao, tunawakaribisha kwa mikono miwili,”amesema.

Pia amemuhakikishia balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili.  

Kwa upande wake Balozi Yahel amesema watalii kutoka nchini Israel wameongezeka kutokana na kuvutiwa na mazingira mazuri ya amani na utulivu wa nchi.

Balozi Yahel amesema atakuwa mjumbe wa kuitangaza Tanzania popote duniani.