Sera duni kikwazo cha mapato sekta ya maliasili

Muktasari:

Utafiti uliofanywa na Oxfam USA kupitia nchi nne za Ghana, Peru, Tanzania na Senegal umeonyesha fursa na changamoto zilizopo kwa taasisi za ndani katika usimamizi wa mapato kwenye sekta ya madini.

Dar es Salaam. Sekta ya maliasili imeshindwa kuchangia pato kubwa kwa Serikali kutokana na sera duni, ripoti ya Weak Link imeonyesha.

Utafiti uliofanywa na Oxfam USA kupitia nchi nne za Ghana, Peru, Tanzania na Senegal umeonyesha fursa na changamoto zilizopo kwa taasisi za ndani katika usimamizi wa mapato kwenye sekta ya madini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti huo uliofanywa kuanzia Oktoba 2014 hadi Julai 2015, mtafiti wa The Weak Link kutoka Oxfam Tanzania, Dk Martin Kijazi alisema  umeonyesha Tanzania inakabiliwa na umaskini mkubwa.