Serikali kuokoa Sh4bn ikihamia Dom- Chauma

Picha na mtandao

Muktasari:

Akizungumza jana, Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Kayumbu Kabutale alisema uamuzi huo unatekeleza ibara ya 18 ya ilani ya Chauma ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Dodoma. Chama cha Umma (Chauma) kimeunga mkono uamuzi wa Serikali kuhamia mjini hapa, kwa kuwa utaokoa zaidi ya Sh4 bilioni zilizokuwa zikipotea kila siku kutokana na msongamano wa watu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana, Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Kayumbu Kabutale alisema uamuzi huo unatekeleza ibara ya 18 ya ilani ya Chauma ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

“Katika Ilani ya uchaguzi ya chama chetu ambayo tuliiuza mwaka jana tulieleza kuwa kama tukichaguliwa tutahamishia makao makuu mjini hapa. Kwa hiyo sisi tunafurahia uamuzi huu maana ni utekelezaji wa ilani yetu,” alisema Kabutale.

Alisema mji wa Dodoma una watu wasiozidi 500,000 wakati Dar es Salaam ni zaidi ya milioni nne, hivyo kuwa na msongamano ambao unaepukika.