Serikali ya Tanzania yatoa tahadhari mlipuko wa Ebola

waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watooto Umm Mwalimu akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusia na ugonjwa wa Ebola. Picha na Anthony Siame

Muktasari:

Mikoa iliyo hatarini kupata ugonjwa huo ni ile ya mipakani Mwanza, Kagera, Katavi, Rukwa na Songwe.

 


Dar es Salaam. Serikali imetoa tahadhari kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini baada ya watu 91 kuugua DRC Congo na wengine 50 kufariki dunia.

Idadi hiyo imeongezeka kutoka wagonjwa 26 katika mlipuko uliotokea Julai mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Agosti 21 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema nchi ipo hatarini kupata ugonjwa huu kwa sababu ya ujirani kati ya Congo na Tanzania lakini mpaka sasa bado haujaingia nchini Tanzania.

Ameitaja mikoa ambayo ipo hatarini kuwa ni pamoja na Mwanza, Kagera, Katavi, Rukwa na Songwe ambayo ipo mipakani.

Huo ni mlipuko wa 10 kutokea nchini DRC Congo huku  wastani wa wanaoambukizwa na wanaofariki ukitajwa kuwa ni wa  kiwango cha  asilimia 50.