Friday, February 17, 2017

Serikali yapiga marufuku vyeti vya zamani vya homa ya manjano

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari,Kushoto ni Mganga Mkuu wa serikali,Profesa Mohammed Kambi na Mkurugenzi wa Huduma za uhakiki na ubora wa Huduma,Dk Mohammed Mohammed. Picha na Herieth Makweta 

By Herieth Makwetta, Mwananchi

Dar es Salaam. Serikali imesema haitatambua vyeti vya zamani vya homa ya manjano na yeyote atakayekutwa nacho litakuwa ni kosa la jinai.

Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali ilishaanza kutoa chanjo mpya inayodumu kwa muda mrefu na ile ya maisha.

"Chanjo inayotolewa sasa ni ile ya miaka 10 na ya maisha kwa yule ambaye hajachanjwa afike na pasi yake ya kusafiria ili apate huduma hii, gharama ni Sh 5,000 kwa Mtanzania na Dola 10 kwa raia wa nje," alisema.

-->