Thursday, June 14, 2018

Serikali yapunguza kodi ya kampuni

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi 

By Julius Mathias, Mwananchi

Dodoma. Katika juhudi za kuvutia uwekezaji nchini, Serikali imetangaza kupunguza kodi ya faida inayotozwa kwa kampuni kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 20 ndani ya miaka mitano ijayo.

Punguzo hilo limetangazwa leo, Juni 14 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Napendekeza kushusha kiasi cha (kodi ya faida) corporate tax kutoka asilimia 30 mpaka 20 ndani ya miaka mitano ijayo kuanzia 2018/19 mpaka 2022-23,” amesema Dk Mpango.

Uamuzi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.

 

 


-->