Serikali yatafiti hali ya upatikanaji umeme

File Photo

Muktasari:

 Meneja wa Takwimu Mkoa wa Kigoma, Moses Kahero juzi aliwataka viongozi wa ngazi zote kuhamasisha wananchi kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakapofika maeneo yao kwa ajili ya kukusanya taarifa.

Kigoma. Wakala wa Umeme Vijijini (Rea)  kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inafanya utafiti kuhusu hali ya upatikanaji wa nishati nchini.

Meneja wa Takwimu Mkoa wa Kigoma, Moses Kahero juzi aliwataka viongozi wa ngazi zote kuhamasisha wananchi kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakapofika maeneo yao kwa ajili ya kukusanya taarifa.

Alisema utafiti huo utahusisha maeneo 26 yaliyochaguliwa kitaalamu na kila eneo zitahojiwa kaya 15 na kwamba, lengo la Serikali  ni kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali ya upatikanaji wa umeme katika ngazi ya kaya.