Serikali yawaonya wakimbizi Katumba

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ametoa onyo hilo leo wakati akiwahutubia wananchi hao wanaoishi  kwenye makazi ya  wakimbizi ya   Katumba, kwenye  mkutano  wa  hadhara  uliofanyika katika Kijiji  cha Nduwa.

Muktasari:

Sumbawanga. Serikali imewaonya na kuwatahadharisha  raia wake wapya ambao awali walikuwa wakimbizi  wanaoishi  katika  makazi  ya  Katumba  wilayani Mpanda mkoani Katavi kuwa itawachukulia hatua za kisheria wale wote ambao wanaingiza silaha na kufanya  vitendo vya ujambazi na ujangili.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ametoa onyo hilo leo wakati akiwahutubia wananchi hao wanaoishi  kwenye makazi ya  wakimbizi ya   Katumba, kwenye  mkutano  wa  hadhara  uliofanyika katika Kijiji  cha Nduwa.
Amesema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama, haitasita kuwachukulia  hatua  kali za kisheria wale wote  watakaobainika kufanya hivyo  kwani kupewa uraia wa hapa nchini sio  sababu ya  wao   kufanya   vitendo uhalifu na ujangili unaotishia kumaliza rasilimali zetu.
Masauni amesema taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba  baadhi raia hao wapya waliopewa  uraia miaka ya karibuni wamekuwa sio waaminifu na vinara wa vitendo vya uhalifu hususani ujangili na ujambazi wa kutumia silaha za moto.