Wednesday, March 15, 2017

Serukamba aishauri Serikali

By Elizabeth Edward na Zulfa Musa

Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba ameitaka Serikali kuangalia upya suala la kuelekeza taasisi zake kupeleka mapato yake yote hazina kwani linachangia kukwama kwa shughuli zinazohitaji fedha.

Serukamba ametoa kauli hiyo wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kukuta bweni la wanafunzi (Hall 2) likiwa limefungwa kutokana na uchakavu kupita kiasi.

Bweni hilo linalopaswa kuchukua wanafunzi 396 limeshindwa kukarabatiwa kutokana na kukosekana kwa fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Amesema  endapo chuo hicho kingeachiwa sehemu ya mapato yake kingeweza kufanya ukarabati huo bila kusubiri ruzuku ya serikali ambayo haijatolewa kwa muda mrefu.

"Nadhani taasisi kama vyuo na hospitali ziachiwe mapato yake ili yasaidie kwenye shughuli za maendeleo ,"amesema Serukamba.

-->