Sh10 bilioni zahitajika ujenzi wa ofisi ya RC Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa DODOMA, JORDAN RUGIMBANA

Muktasari:

Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Shally Raymond amesema hakuna mpango wa makusudi wa kumaliza ujenzi wa jengo hilo ambalo lilianza kujengwa miaka 9 iliyopita.

Dodoma. Imeelezwa kuwa Sh10 bilioni zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma lakini uwezekano wa kukamilika mapema bado ni ndoto.

Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Shally Raymond amesema hakuna mpango wa makusudi wa kumaliza ujenzi wa jengo hilo ambalo lilianza kujengwa miaka 9 iliyopita.

Jana kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (PAC) ilibaini changamoto kubwa ya uhaba wa fedha katika mradi huo na kueleza masikitiko yao ya namna ambavyo jengo hilo limeshindwa kupewa kipaumbele.

Raymond ameeleza namna Serikali inavyotenga fedha hizo, inaonyesha wazi kuwa hakuna juhudi za makusudi na kimkakati kumaliza ujenzi.

Ameshangazwa kuwa licha ya Serikali kutangaza nia ya kuhamia Dodoma, lakini wameshindwa kutoa kipaumbele kwa mkoa wa Dodoma kumaliza ujenzi.