Sh229 milioni kujenga Kituo cha Polisi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ametembelea ujenzi kituo cha kisasa cha polisi katika Mji Mdogo wa Mbalizi .

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa Mji mdogo wa Mbalizi,   Kassim Ugulumo amesema hayo leo (Jumapili) alipotoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipotembelea ujenzi wa kituo hicho unaofanywa na wananchi.

Mbeya. Zaidi ya Sh 229 milioni zitatumika kujenga kituo cha kisasa cha polisi katika Mji Mdogo wa Mbalizi mkoani hapa ili kukidhi haja za kuwa wilaya ya kipolisi.

Mkurugenzi wa Mji mdogo wa Mbalizi,   Kassim Ugulumo amesema hayo leo (Jumapili) alipotoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipotembelea ujenzi wa kituo hicho unaofanywa na wananchi.

Ugulumo amesema kituo hicho kinajengwa  Mtaa wa Utengule Usongwe katika eneo la ekari tatu ambazo wananchi walizitoa kwa hiari kujenga kituo hicho.

Ugulumo amsema  wazo la wananchi hao kufikia ya kuisaidia Serikali yao inatokana na ukweli kwamba mji wa Mbalizi unakua kwa kasi hivyo upo uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa matukio ya kihalifu.