Shaffih Dauda, MC Luvanda washikiliwa na polisi

Muktasari:

Makosa ya kuendesha mitandao ya kijamii bila kusajili maudhui, yanadaiwa kuwaponza mtangazaji Shaffih na MC Luvanda baada ya kudakwa na polisi na kuwekwa mahabusu tangu Ijumaa iliyopita.

Dar es Salaam.  Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wanadaiwa kuwashikilia mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Clouds, Shaffih Dauda na MC Luvanda kwa kile kinachodaiwa kumiliki mitandao ya Youtube bila kusajili maudhui.

Mwingine aliyekamatwa katika sakata hilo ni pamoja na msimamizi wa mtandao wa Youtube wa Shaffih, anayejukana kwa jina Ben Ali, maarufu kwa jina la Ben On Air.

Taarifa iliyopatikana usiku huu wa Septemba 18, kutoka kwa watu wa karibu wa Shaffih zinadai mtangazaji huyo na wenzake hao walikamatwa tangu Ijumaa iliyopita na kufikishwa kituo cha polisi cha Mabatini kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi  wanakoshikiliwa hadi sasa.