Shehena ya bidhaa yakamatwa bandari bubu

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba

Muktasari:

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema jana kuwa shehena ya bidhaa hizo ilikamatwa saa tisa usiku wa kuamkia jana katika Bandari bubu ya Kigombe, wilayani Muheza.

Muheza. Shehena ya bidhaa kutoka nje zinazodaiwa kuingizwa zikiingizwa nchini kwa magendo kupitia bandari bubu ya Kigombe¸ imekamatwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema jana kuwa shehena ya bidhaa hizo ilikamatwa saa tisa usiku wa kuamkia jana katika Bandari bubu ya Kigombe, wilayani Muheza.

Polisi kwa kushirikiana na Idara ya Forodha ya Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga, ndio waliofanikisha kukamatwa kwa shehena hiyo.

Alitaja bidhaa hizo kuwa ni mifuko 64 ya sukari kutoka nchini Brazil kila mmoja una uajazo wa kilo 50, madebe 304 ya mafuta ya chakula kutoka Indonesia kila moja lina ujazo wa lita 20 na mifuko 10 ya mchele kutoka Pakistan.