Sheria ya gesi itawasaidia wazawa

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Merdard .

Muktasari:

  • Alisema hayo wakati wa kufungua mkutano wa wadau wa Sekta ya Gesi. Katika mkutano huo, Benki ya Dunia imezindua ripoti yake kuhusu uwekezaji na ushiriki wa watanzania Katika huduma na bidhaa.

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Merdard Kalemani amesema wazalishaji wa ndani watakuwa na uhakika wa  kuuza bidhaa zao kwa asilimia 25 katika kampuni za kigeni baada ya kuwa na Sheria, Sera ya Gesi pamoja na ushirikishwaji na uwezeshaji wazawa.Alisema sera hiyo itazalisha ajira zitakuwa nyingi.

Alisema hayo wakati wa kufungua mkutano wa wadau wa Sekta ya Gesi. Katika mkutano huo, Benki ya Dunia imezindua ripoti yake kuhusu uwekezaji na ushiriki wa watanzania Katika huduma na bidhaa.

"Baada ya kuwa na Sheria, Sera ya Gesi pamoja na sera ya wazawa (LCP), kanuni zinaandaliwa na sasa mchakato uko sehemu nzuri ya ushiriki wa wadau,"alisema.