KUELEKEA DODOMA: Shibuda: Mifuko ya jamii ijenge nyumba Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama cha Ada Tadea, John Shibuda

Muktasari:

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana Shibuda, alimpongeza Rais Dk John Magufuli kwa uamuzi wa kuhamia Dodoma, kutekeleza ahadi ya Serikali ya Awamu ya Kwanza.

Dodoma. Katibu Mkuu wa Chama cha Ada Tadea, John Shibuda ameishauri Serikali kuzungumza na mifuko ya hifadhi ya jamii, ijenga nyumba za watumishi wa umma watakao hamishiwa mjini hapa.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana Shibuda, alimpongeza Rais Dk John Magufuli kwa uamuzi wa kuhamia Dodoma, kutekeleza ahadi ya Serikali ya Awamu ya Kwanza.

“Naishauri Serikali kufanya mazungumzo na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kujenga nyumba za watumishi,” alisema.

Mwanachama wa Jumuiya ya Wenye Viwanda, Wafanyabiashara na Kilimo nchini (TCCIA), Fred Azaria alisema ujio wa makao makuu Dodoma, utaongeza fursa nyingi za kibiashara katika mji huo.

“Kuwepo kwa maeneo ya wafanyabiashara ni fursa kwetu ya kukuza biashara zetu. Tutashirikiana na Serikali kuhakikisha hili linatekelezwa,”alisema.