Shule Muheza yakosa madarasa, madawati

Muktasari:

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 354, John Ngadallah amewaambia waandishi wa habari kwamba pia wanakabiliwa na uhaba wa madawati hali inayowafanya wasome wakiwa wamekaa chini.

Muheza, Tanga. Wanafunzi 122 wa Shule ya Msingi ya Machemba wilayani hapa wanasomea chini ya mti kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa na mvua inaponyesha masomo husimama.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 354, John Ngadallah amewaambia waandishi wa habari kwamba pia wanakabiliwa na uhaba wa madawati hali inayowafanya wasome wakiwa wamekaa chini.

Mwenyekiti wa Serikali ya kitongoji, Said Juma, amesema wameitisha mkutano wa kijiji na kukubaliana kila kaya kuchangia matofali matatu kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo.