Shule ya Msingi Kombo yapokea mifuko ya saruji

Muktasari:

Amekabdhi mifuko hiyo leo (jumatano) mbele ya kamati ya shule na kusema ni moja ya hatua ya kutatua changamoto za madarasa chakavu yaliyojengwa tangu mwaka 1974.

Dar es Salaam. Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omari Kumbilamoto amekabidhi mifuko mitano ya saruji katika shule ya msingi Kombo iliyoko kata ya Vingunguti kwa ajili ya ukarabati wa chumba cha darasa. 

Amekabdhi mifuko hiyo leo (jumatano) mbele ya kamati ya shule na kusema ni moja ya hatua ya kutatua changamoto za madarasa chakavu yaliyojengwa tangu mwaka 1974. 

Pamoja na mifuko hiyo amekabdhi   ndoo tano na makopo saba ya rangi ili kuboresha muonekano wa shule hiyo kongwe iliyoko katika kata ya vingunguti. 

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Stella Mhando amesema wana furaha kuona viongozi wanaguswa katika kuleta maendeleo ya elimu hasa kukarabati miundombinu.