CCM yapitisha wagombea ubunge

Friday August 14 2015

Mwanachama wa CCM, Khadija Limbumba akiwa na

Mwanachama wa CCM, Khadija Limbumba akiwa na karatasi yenye picha za wanaowania kuteuliwa cha chama hicho kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga, alipokwenda kupiga kura katika Kituo cha Tawi la Kilimo baada ya kurudiwa kwa uchaguzi wa jimbo hilo, Dar es Salaam jana. Picha na Anthony Siame 

By Waandishi Wetu, Mwananchi

Katika jimbo la Pangani Vijijini, mgombea aliyeshika nafsi ya pili, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita alipitishwa badala ya John Sallu aliyeongoza.Kwa upande wa viti maalumu, Halmashauri Kuu imefanya mabadiliko katika baadhi ya mikoa ikiwamo Dar es Salaam ambao aliyeongoza, Angela Kizigha aliondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Janeth Masaburi.

Katika kundi la vijana, mcheza filamu Irene Uwoya ambaye alishindwa katika Baraza Kuu la UWT, sasa ameibukia katika nafasi ya sita huku jina la Julia Didas Masaburi likiondolewa katika orodha hiyo.

Katika  Taasisi zisizokuwa za kiserikali, jina la Ritha Mlaki limeondolewa na nafasi yake kupewa Khadija Hassan Aboud ili kuweka uwiano wa Muungano na sasa ataungana na Dk Getrude Rwakatare katika kundi hilo.

Vilevile, katika uteuzi huo, yameibuka majina mawili  ya waliokuwa wanachama wa Chadema, akiwamo Juliana Shonza aliyeteuliwa viti maalumu kupitia Mkoa wa Songwe na Filipa Mturano kupitia Mkoa wa Kigoma.

Mwamoto ambwaga Profesa Msolla

Ndoto za Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msolla kurudi bungeni zimefutika baada ya kushindwa katika marudio ya uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika juzi.

Katika uchaguzi huo uliowashirikisha watiania 15, Venance Mwamoto aliibuka mshindi baada ya kupata kura 13,713 wakati mshindani wake, Profesa Msolla akipata kura 9,810.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo, Clemence Mponzi alimtangaza Mwamoto kuwa mshindi wa uchaguzi huo ambao awali, Profesa Msolla aligomea matokeo ya awali na kukata rufaa. Juzi, Profesa Msolla alikubali matokeo na kusaini fomu muda mfupi baada ya kutangazwa.

Wagombea wengine walioshiriki uchaguzi huo ni Danford Mbilinyi (1,142), Chelestino Mofuga (576), Ashiraf  Chusi (28), Merick Luvinga (161) ,Tadei Kikoti (136), Anosta  Nyamonga (68), Yefred Myenzi (63), Luciano  Mwambosa (53), Mgabe Kihongosi (46), Abdul Mkakatu (28), France Mkokwa (47), Basike Mteleka (17) na Israel Salufu (9).

Rufiji

Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura za maoni kwa marudio jana ilipungua ikilinganishwa na ilivyokuwa katika uchaguzi uliofanyika Agosti Mosi.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Rufiji, Musa Nyelesa alikiri kupungua idadi ya wapigakura katika jimbo hilo ikilinganishwa na uchaguzi uliopita akisema: “watu wamesusia kwa malengo yao binafsi.”

Ukonga

Msimamizi  wa uchaguzi wa marudio Jimbo la Ukonga, alilazimika kuwatimua wajumbe wa Kamati ya Siasa Tawi la Gongo la Mboto waliopiga kambi katika kituo hicho ili kuwaelekeza wanachama mgombea wa kumpigia kura.

Msimamizi huyo, Seif Fundikira alisema wajumbe hao walipoingia katika kituo hicho walikataa kutoka na baada ya kuwachunguza alibaini kuwa walikuwa wakiwaelekeza wanachama ni mgombea gani wa kumpigia kura.”

Imeandikwa na Habel Chidawali, Sharon Sauwa (Dodoma) na Geofrey  Nyang’oro (Iringa).

Advertisement