Monday, June 24, 2013

Majeshi ya A. Kusini yatua DRC

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Majeshi ya Afrika Kusini yameingia Jamhuri ya Kidemokasia ya Congo kuunganisha nguvu katika Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa Mashariki mwa nchi hiyo kwenye mji wa Goma.

Majeshi hayo yenye wapiganaji 1,345 yanaingia DRC ikiwa siku tano baada ya Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe kuliambia gazeti hili katika mahojiano mafupi kuwa Afrika Kusini na Malawi hazijapeleka vikosi vyao timilifu Mashariki mwa DRC.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC, Ebrahim Ebrahim alisema mwishoni mwa wiki kuwa Afrika Kusini imeshaleta askari wake ambao wataungana na Tanzania na Malawi kwa ajili ya kulinda  amani kwenye mji huo. Jumla askari wa Umoja wa Mataifa wanaotarajiwa ni 3,000.

Ebrahim alisema kuwa wanajeshi wa Tanzania tayari wameshawasili kwenye mji huo. Kikosi cha kwanza cha Tanzania kilikuwa cha wapiganaji 100 kati ya 850 wanaotarajiwa kuunganisha nguvu kupambana na waasi wa M23.

-->