Sido yawajengea uwezo wenye ulemavu

File Photo

Muktasari:

Mafunzo hayo yaliyolenga kutoa mbinu ya ujasiriamali kwa kundi hilo, yalihudhuriwa na washiriki 45 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera.

Mwanza. Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (Sido), Mkoa wa Mwanza limetoa mafunzo ya ufugaji wa kuku na utengenezaji vikapu kwa watu wenye ulemavu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mafunzo hayo yaliyolenga kutoa mbinu ya ujasiriamali kwa kundi hilo, yalihudhuriwa na washiriki 45 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera.

Ofisa Biashara wa Sido Mkoa wa Mwanza, Maneno Maporo alisema mafunzo hayo ni utekelezaji wa mradi wa Kuwainua Watu Wenye Ulemavu.