Siri ya Serikali kuhakiki vyeti yabainika

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angela Kairuki

Muktasari:

Tangu uhakiki huo uanze mapema mwaka huu, zaidi ya watumishi 1,000 wamekutwa na vyeti vya kughushi.

Dar es Salaam. Uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma ambao umewaweka wengi wao roho juu utakuwa ufunguo wa kuboreshewa masilahi na kupanda madaraja kwa watakaofuzu na kutoa fursa ya ajira mpya, imebainika.

Tangu uhakiki huo uanze mapema mwaka huu, zaidi ya watumishi 1,000 wamekutwa na vyeti vya kughushi.

Wafanyakazi wengi wa Serikali, idara za Serikali, wakala, mashirika na taasisi mbalimbali za umma wamekuwa wakihaha kutafuta vyeti vyao Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) na wanaoamini wamevipoteza kwa njia mbalimbali wamelazimika kutangaza kwenye magazeti ama kwa lengo la kupatiwa vingine au kutumia taarifa hiyo kueleza upotevu huo.

Hata hivyo, baadhi ya walioghushi au kutumia vya wenzao wameripotiwa kuacha kazi na kutokomea.

Habari zinazihusiana