St. John’s watoa wahitimu 170 wa ugavi wa dawa

Muktasari:

  • Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mbennah alisema juzi kuwa kozi hiyo ilianzishwa baada ya St John’s na Mradi wa Tuimarishe Afya Health Promotion Systems Support (HPSS) kufanya utafiti na kubaini upungufu wa wagavi wa dawa.

 Kwa mara ya kwanza Chuo Kikuu cha St. John’s kimetoa wahitimu 171 wa kozi ya utaalamu wa ugavi wa dawa.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mbennah alisema juzi kuwa kozi hiyo ilianzishwa baada ya St John’s na Mradi wa Tuimarishe Afya Health Promotion Systems Support (HPSS) kufanya utafiti na kubaini upungufu wa wagavi wa dawa.

Mbennah alisema kuwapo kwa mradi wa HPSS kumewezesha chuo hicho kuimarisha maabara ambayo imefanikiwa kuajiri wakufunzi wawili na kufadhili wanafunzi ili kuwawezesha kusoma kozi hiyo ambayo imekuwa muhimu kwa afya ya binadamu.

Mshauri wa huduma katika mradi wa HPSS, Ali Kebi alisema tafiti mbalimbali zilizofanyika kabla ya kuanzishwa kwa kozi hiyo zilionyesha kuwapo wa uhaba wa kada hiyo muhimu kwa afya ya mwanadamu.

Alisema kitendo cha kugawa dawa kwa watu wasiokuwa na sifa ni hatari kwa maisha ya wagonjwa na watumiaji wa dawa za hospitali lakini kwa waliomaliza wanakuwa mfano mzuri kwa wengi.

Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Profesa Penina Mlama alisema jumla ya wahitimu 1,266 walihitimu katika mahafali hayo yakiwa ni ya nane tangu kuanzishwa kwa St. John’s 2007.