Startimes yaongeza mnara jijini Tanga

Muktasari:

Meneja wa Startimes Kanda ya Pwani, David Kisaka alisema: “Mwonekano haukuwa wa kuridhisha. Tunaushukuru uongozi wa halmashauri ya jiji kwa kutupa eneo la kuweka mnara huu wenye nguvu zaidi ya ule wa mwanzo.” .

Tanga. Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes imezindua mnara wa mawasiliano Tangamano ili kuboresha huduma zake kwa wateja wa Mkoa wa Tanga.

Meneja wa Startimes Kanda ya Pwani, David Kisaka alisema: “Mwonekano haukuwa wa kuridhisha. Tunaushukuru uongozi wa halmashauri ya jiji kwa kutupa eneo la kuweka mnara huu wenye nguvu zaidi ya ule wa mwanzo.” .

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Thobias Mwilapwa alisema: “Teknolojia ni muhimu kufanikisha mapinduzi ya viwanda ...tunaahidi kutoa ushirikiano kwa Startimes.”