Sungusungu kurejeshwa Mwanza

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alitangaza mpango huo kwenye Kijiji cha Katunguru wilayani Sengerema, alipotembelea miradi inayotekelezwa na wananchi kwa ufadhili wa Mradi wa Hifadhi na Usimamizi wa Bonde la Ziwa Victoria (Lvemp II).

Sengerema. Mkoa wa Mwanza unakusudia kufufua ulinzi wa jadi wa Sungusungu ili kusaidiana na Jeshi la Polisi kudhibiti uhalifu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alitangaza mpango huo kwenye Kijiji cha Katunguru wilayani Sengerema, alipotembelea miradi inayotekelezwa na wananchi kwa ufadhili wa Mradi wa Hifadhi na Usimamizi wa Bonde la Ziwa Victoria (Lvemp II).

 “Kuanzia sasa kila mkuu wa wilaya aorodheshe majina ya waliokuwa watemi na makamanda wa Sungusungu waliopo eneo lake,” alisema Mongella.

Alisema askari hao wa jadi wataundiwa miongozo na utaratibu wa utekelezaji wa majukumu yao.