TADB yavikopesha Sh 6.5bilioni vikundi 20 vya wakulima

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga

Muktasari:

  • Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga wakati wa utiaji saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na Benki hiyo katika hafla iliyofanyika Ofini kwa Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanikiwa kukopesha jumla ya shilingi bilioni 6.5 kwa vikundi 20 vyenye jumla ya wakulima 2575 ili kuisaidia Serikali katika kujenga Tanzania ya viwanda.

Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga wakati wa utiaji saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na Benki hiyo katika hafla iliyofanyika Ofini kwa Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.