TCRA yatoa leseni 45 za watoa huduma mitandaoni

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba

Muktasari:

Yasema waombaji waliokuwa 262

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa leseni 45kwa watoa huduma wa maudhui mitandaoni.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 25, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema kulikuwa na waombaji wa leseni 262.

Amesema waombaji 65 wametimiza vigezo kati yao 45 wamelipia na ndiyo waliopewa leseni leo.

Kilaba amesema wanaendelea kupokea maombi na  wataendelea kutoa leseni kwa watakaotimiza vigezo.