TCRA yatoa leseni 45 za watoa huduma mitandaoni
Muktasari:
Yasema waombaji waliokuwa 262
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa leseni 45kwa watoa huduma wa maudhui mitandaoni.
Akizungumza leo Ijumaa Mei 25, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema kulikuwa na waombaji wa leseni 262.
Amesema waombaji 65 wametimiza vigezo kati yao 45 wamelipia na ndiyo waliopewa leseni leo.
Kilaba amesema wanaendelea kupokea maombi na wataendelea kutoa leseni kwa watakaotimiza vigezo.