TCU yakiri dosari taarifa ya wanafunzi 8,357

Muktasari:

  • Taarifa kutoka  TCU  kwa vyombo vya habari imesema kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali ,tume sasa itaendelea kuwasiliana  moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha zoezi hilo.

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu  Tanzania ( TCU)

imetoa ufafanuzi   kuhusu  wanafunzi 8,357 waliotajwa  kuwa hawana sifa stahiki  za kuendelea na elimu ya juu na kudai kwamba kulikuwa na dosari katika taarifa zao.

Taarifa kutoka  TCU  kwa vyombo vya habari imesema kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali ,tume sasa itaendelea kuwasiliana  moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha zoezi hilo.

Taarifa hiyo imesema  wanafunzi wote walioorodhesha  katika taarifa iliyotolotewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea  na masomo yao ya kawaida.

“TCU inapenda kuuarifu umma  kuwa ,uhakiki wa ubora  wa wanafunzi wa elimu ya juu hufanyika kwa mujibu wa kifungu 5(1)(b)c) cha Sheria ya Vyuo vikuu Sura ya 346 YA Sheria za Tanzania,’’imesema taarifa hiyo.