TPSF yataka kero bandarini Dar kushughulikiwa

Muktasari:

Kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi ameiomba Serikali kuendelea kushughulikia kero za ukusanyaji wa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza leo Jumatatu Machi 19, 2018 katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara, Mengi amesema taasisi hiyo imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu mfumo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia utaratibu wa kujikadiria ukusanyaji wa mapato.

“Tumekuwa tukipokea malalamiko ya wafanyabiashara, tunapongeza sana juhudi za rais (John Magufuli) kwa sababu maduka mengi yalikuwa yanafungwa kwa sababu ya kodi,” amesema Mengi.

Mengi amesema TPSF ina matarajio kwamba Serikali itaendelea kuimaisha ushirikiano na wafanyabiashara nchini.