TRA yakusanya Sh 7.27 trilioni nusu mwaka

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo

Muktasari:

  • Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 12.74 ikilinganishwa na Sh 6.4 trilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliopita.
  • Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema kiasi hicho kimeweza kukusanywa kutokana na jitihada mbalimbali ikiwemo kuboresha mifumo ya ukusanyaji.

Dar es Salaam.Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya Sh 7.27 trilioni katika nusu ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 12.74 ikilinganishwa na Sh 6.4 trilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliopita.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema kiasi hicho kimeweza kukusanywa kutokana na jitihada mbalimbali ikiwemo kuboresha mifumo ya ukusanyaji.

Alisema TRA imeendelea kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuongeza ufanisi kwenye ufuatiliaji na ukusanyaji wa kodi.

"Tunajitahidi tufikie lengo tulilojiwekea kwa mwaka huu wa fedha la kukusanya Sh15.1 trilioni,"

"Hilo halitakuwa gumu sana kutimia kwa kuwa tumeimarisha mifumo yetu na tumezuia mianya ya watu kukutana kodi zinalipwa kielektroniki," alisema Kayombo.