TRA yawapa elimu ya kodi waumini wa Askofu Gwajima

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Muktasari:

Rose alisema kuwa shughuli za Serikali katika nchi yeyote duniani, ikiwemo Tanzania zinagharamiwa na fedha zinazotokana na kodi pamoja na tozo mbalimbali.

Dar es Salaam. Watanzania wameaswa kujenga utamaduni wa kulipa kodi na kudai risiti pindi wanapofanya biashara au kununua bidhaa ili kuisaidia Serikali kukusanya mapato kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za kijamii.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rose Mahendeka alipokuwa akitoa elimu kwa waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.

Rose alisema kuwa shughuli za Serikali katika nchi yeyote duniani, ikiwemo Tanzania zinagharamiwa na fedha zinazotokana na kodi pamoja na tozo mbalimbali.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewahimiza waumini wake kuishika na kuitumia elimu waliyopata kutoka kwa mwakilishi wa TRA ambapo aliwataka waumini hao kujenga utamaduni wa kudai risiti kila anapofanya malipo ili kusaidia ukusanyaji wa mapato ya Serikali.