Taasisi 9 za serikali zakutwa na viashiria vya rushwa

Muktasari:

Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma(PPRA) Matern Lumbanga.

Dar es Salaam. Taasisi tisa za serikali ikiwamo Taasisi ya Mifupa (MOI), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, zimetajwa kuwa na viashiria vya rushwa.

Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma(PPRA) Matern Lumbanga.

Maeneo matano yaliyoangaliwa ni ukidhi wa sheria ya manunuzi ya umma, ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi, kupima thamani halisi ya fedha ilivyotumika, malipo yenye utata na viashiria vya rushwa.

Hatua hiyo ni matokeo ya ripoti ya ukaguzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma(PPRA) , iliyofanya ukaguzi wa manunuzi ya umma katika kipindi cha mwaka 2015/16 huku ikihakiki ukaguzi wa ukaguzi iliyofanya 2014/15.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, PPRA ilikagua Taasisi 70 kati ya 104 iliyopanga kukagua, mikataba 21,313 ya manunuzi yenye thamani ya Sh. 1.05trilion ilikaguliwa.Jumla ya Taasisi nchini ni 493.