Taasisi ya matibabu ya moyo yapigwa jeki

Muktasari:

  • Akipokea vifaa hivyo leo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema vifaa hivyo vitawezesha kuanzisha chumba cha tatu cha upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo.

 Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umetoa msaada wa vifaa vya chumba cha upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) vyenye thamani ya Sh325 milioni.

Akipokea vifaa hivyo leo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema vifaa hivyo vitawezesha kuanzisha chumba cha tatu cha upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo.

"Naamini kuanzishwa kwa chumba cha tatu cha upasuaji kutawezesha taasisi hii kufanya upasuaji kwa wagonjwa wengi zaidi ikilinganishwa na awali," amesema Ummy Mwalimu.

Naye balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Janem, amesema nchi hiyo itaendelea kusaidia meandeleo ya sekta ya afya nchini. 

Mpaka sasa JKCI imefanikiwa kufanya upasuaji wa kufungua vifua kupitia chumba cha upasuaji (cardiothoracic) kwa wagonjwa 713 tangu mwaka 2015.