Takukuru kukabili rushwa kivingine

Muktasari:

  • Hayo  yameelezwa na Ofisa wa Uelimishaji wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Hobokela Mwandenga wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake leo (Jumatano).
  • “Huu ni mwendelezo wa kampeni yetu ya kupiga vita rushwa kupitia makundi na vilabu mbalimbali kwenye jamii,” amesema Mwandenga.

Mwanza. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Mwanza imeanzisha kampeni kakabiliana na rushwa kwa kutoa elimu kwenye vijiwe vya waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda.

Hayo  yameelezwa na Ofisa wa Uelimishaji wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Hobokela Mwandenga wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake leo (Jumatano).

“Huu ni mwendelezo wa kampeni yetu ya kupiga vita rushwa kupitia makundi na vilabu mbalimbali kwenye jamii,” amesema Mwandenga.

Amesema vilabu vya kupiga vita rushwa mitaani na kwenye makundi maalum ya kijamii vimewezesha elimu ya kubaini viashiria vya rushwa na kupambana na tatizo hilo kufikia vijana wengi kulinganisha na utaratibu wa awali wa kutumia makundi rasmi