Saturday, July 7, 2018

Tamasha la Ziff lazinduliwa

Baadhi ya rai wakigeni wakijumuika pamoja na

Baadhi ya rai wakigeni wakijumuika pamoja na wananchi tofauti katika bustani za Forodhani mjini Unguja kushuhudia uzinduzi wa tamasha la 21 la kimtaifa la filamu Zanzibar (ZIFF) Picha na Muhammed Khamis. 

By Muhammed Khamis, Mwanachi mkhamis@mwananchi.co.tz

Zanzibar. Maandamano ya uzinduzi wa Tamasha la 21 la filamu za Zanzibar (Ziff) yameanza leo jioni Jumamosi Julai 7, 2018.

Maandamano hayo yameanzia katika viwanja vya bustani ya Kisonge hadi Forodhani ambako litafanyika tamasha hilo kwa siku tisa.

Vikundi mbali mbali  vya burudani vimeshiriki katika  maandamano hayo huku vikitoa burudani ya aina yake kwa wageni na wenyeji.

Katika tamasha la mwaka huu, filamu 165 za wasanii mbalimbali barani Afrika zitaonyeshwa.

 

 

-->