Tanesco: Tunalipa kodi zote

Muktasari:

Tanesco imesema mradi huo unaoendelea kujengwa, unahusisha ununuzi na usafirishwaji wa mitambo mingi mikubwa kutoka nje ya nchi, lakini kazi ya ujenzi inaendelea na itakamilika kwa wakati.

Dar es Salaam. Shirika la Umeme (Tanesco), limesema linafuata taratibu zote za kisheria pamoja na kulipia kodi na usafirishaji wa mitambo linayonunua, hivyo mradi wa Kinyerezi II utamalizika kwa wakati.

Tanesco imesema mradi huo unaoendelea kujengwa, unahusisha ununuzi na usafirishwaji wa mitambo mingi mikubwa kutoka nje ya nchi, lakini kazi ya ujenzi inaendelea na itakamilika kwa wakati.

“Hadi kufikia Mei 2017, Tanesco tayari imeshapokea mizigo mingi, ikiwa ni pamoja na makontena zaidi ya 400 ambayo yamepokelewa katika Bandari ya Dar es Saalam (na) tayari yameshafikishwa eneo la Kinyerezi ili kuendelea na ujenzi,” inasema taarifa hiyo.

“Mradi wa umeme wa Kinyerezi II utapokea jumla ya makontena 900 na mizigo mingine mikubwa hadi kufikia mwezi Agosti 2018.”