Tanesco inadai mabilioni, inadaiwa mabilioni

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani akizungumza bungeni alipokuwa akijibu hoja ya wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Mapato ya Tanesco yameongezeka kutoka Sh 29 bilioni kwa wiki na kufikia 32.5 bilioni.


Dodoma.Waziri wa Nishati, Dk Merdad Kalemani amesema Shirika la Umeme Tanzani (Tanesco) linadaiwa Sh938 bilioni.

 Amesema Tanesco inakabiliwa na madeni hayo huku ikidai zaidi ya Sh200 bilioni.

Waziri Kalemani amesema hayo bungeni leo Mei 25, alipokuwa akihitimisha hoja ya bajeti yake kwa mwaka 2018/19.

“Kwa sasa tunafanya uhakiki wa madeni hayo ili kutoa mwelekeo wa nini kifanyike,” amesema.

Amesema  Tanesco kwa sasa limeanza kuimarika kwa kiasi kikubwa na makusanyo ya mapato yake yameongezeka kutoka Sh 29 bilioni kwa wiki na kufikia 32.5 bilioni.

“Lakini Tanzania ipo juu kwa usambazaji wa umeme vijiji ambao umefikia asilimia 49.5,” amesema.