Tanesco yaomba radhi kukatika kwa umeme

Muktasari:

Taarifa ya shirika hilo ilisema kukatika kwa umeme huo ni hitilafu katika gridi ya Taifa.

Dar es Salaam. Shirika la umeme nchini Tanesco limewaomba radhi wateja wake waliopo katika mikoa iliyounganisha na gridi ya taifa kutokana na usumbufu wa kukatikiwa umeme leo asubuhi.

Taarifa ya shirika hilo ilisema kukatika kwa umeme huo ni hitilafu katika gridi ya Taifa.

"Tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea au utakaojitokeza'"ilisema sehemu ya taarifa hiyo 

Umeme ulikatika asubuhi saa 12:30 katika mikoa hiyo.