Tanga wapinga bei ya maji

File Photo

Muktasari:

Wakizungumza kwenye mkutano wa wadau wa watumia maji uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri na kuishirikisha Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) na Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda wakazi hao wamesema ongezeko hilo halizingatii hali halisi ya maisha yao.

Korogwe. Wakazi wa Halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga, wameijia juu Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Kuwassa) kwa kutoa pendekezo la kuongeza bei ya maji kwa asilimia 166.

Wakizungumza kwenye mkutano wa wadau wa watumia maji uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri na kuishirikisha Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) na Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda wakazi hao wamesema ongezeko hilo halizingatii hali halisi ya maisha yao.

Mamlaka hiyo imependekeza kuongeza bei ya maji kwa ndoo 50 za lita 20 kutoka Sh490 hadi Sh1,213.

Akisoma maoni ya Baraza la Ushauri la Watu Huduma Maji la Ewura (Ewura CCC), Angela Temi amesema nalo lilipinga ongezeko hilo na kuitaka Kuwassa kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo vya uhakika badala ya kupandisha bei ya maji.