Tanroads yaagizwa kuondoa matuta barabara kuu

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni 

Muktasari:

Pia, ameitaka kutengeneza na kurekebisha barabara na kuweka alama na michoro stahiki ili kuzuia ajali zisizo za lazima.

Geita. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ametaka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kutoa matuta yaliyopo kwenye barabara kuu kwa kuwa yanachangia ajali kwa vyombo vya moto.

Pia, ameitaka kutengeneza na kurekebisha barabara na kuweka alama na michoro stahiki ili kuzuia ajali zisizo za lazima.

“Ili kumaliza tatizo la ajali, Kikosi cha Usalama Barabarani kinapaswa kuongezewa nguvu na kuimarishwa, wamiliki wa magari wanatakiwa kuhakikisha yako vizuri kiufundi na madereva wakatae kuendesha magari yenye upungufu,” amesema.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetakiwa kukagua vifaa vya magari ili kujua usalama wake.