Tanzania, Uganda zaongeza kasi ujenzi bomba la mafuta

Serikali za Tanzani na Uganda zimefanya makubaliano ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa bomba la mafuta ya kutoka Hoima hadi Tanga ili ifikapo mwaka 2020 uwe umekamilika. Picha ya Mtandao.

Muktasari:

  • Makubaliano hayo yamefanyika leo katika mkutano wa tatu wa mawaziri wa wizara zinazoshughulikia nishati wa Tanzani na Uganda  uliofanyika mjini Tanga.

Tanga. Serikali za Tanzani na Uganda zimefanya makubaliano ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa bomba la mafuta ya kutoka Hoima hadi Tanga ili ifikapo mwaka 2020 uwe umekamilika.

Makubaliano hayo yamefanyika leo katika mkutano wa tatu wa mawaziri wa wizara zinazoshughulikia nishati wa Tanzani na Uganda  uliofanyika mjini Tanga.

Wakizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano hayo,mwaziri hao walisema mkutano huo umewapa nguvu ya kutekeleza kwa kasi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka ziwa Albert hadi bandari ya Tanga.

Waziri huyo ambaye jana alitembelea bandari ya Tanga, bohari ya mafuta ya GBP Tanzania Limited iliyopo jijini hapa pamoja na Kijiji cha Chongoleani eneo ambalo litaishia bomba la mafuta alisema ameridhishwa na namna maandalizi yalivyoanza.

“Nitakwenda kumpa salamu Rais Museveni kwamba nimekutana na  wananchi wa Tanga na wako tayari kuupokea mradi huu ambao ni muhimu kwa uchumi wa nchi zote mbili”alisema waziri Irene Muloni wa Uganda.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo alisema katika mkutano huo yalijadiliwa  masuala ya uwekezaji, barabara, bandari, usalama, muundo wa timu ya uwekezaji mradi na kampuni itakayoundwa kuendesha mradi huo wa bomba la mafuta.